Kijitabu hiki, kilichoandikwa kwa mpango wa mazungumzo kuhusu Nyama ya Nguruwe, kiliandikwa na Sayyid Saeed Akhtar Rizvi. Katika kijitabu hiki, mwandishi amepinga vikali sana kuhusu kula Nyama ya Nguruwe, akitoa sababu za kisayansi na za kidini, ili kulithibitisha jambo hili, ametumia ripoti za kiganga na za kijamii ambazo zinathibitisha wazi wazi bila ya kubakisha shaka yoyote ile juu ya athari mbaya za Nyama ya Nguruwe kwa afya na uadilifu wa mwanadamu.